Business
Mgawanyiko wa viongozi katika soko la Kongowea wachipuka tena

Mgawanyiko wa viongozi katika soko la Kongowea unazidi kushuhudiwa huku viongozi hao wakitaka kuonyeshana ubabe.

Kulingana na wanabiashara wa eneo hilo, mgawanyiko huo umechangia pakubwa kudhorora kwa maendeleo sokoni humo, pia kujenga chuki miongoni mwao.

Soko hilo lina viongozi sita. Yaonekana kuna mgawanyiko kati yao. Maana mwenyekiti na katibu wake wana muelekoeo tofauti

Kwa upande wake, aliyekua mwenyekiti wa soko hilo Ali Mtsumi alikashifu hatua hiyo na kuitaja kama ubinafsi miongoni mwa viongozi hao wateule.

“Viongozi wa sasa wanaendeleza chuki na kutatiza biashara katika soko hili,'' alisema Mstumi.

Itakumbukwa kuwa aliyekua mwenyekiti wa soko hilo Daniel Ndunga Ndii alifariki mapema mwaka wa 2016 kukiwa tayari na mgawanyiko sokoni humo. 

Report Story
Recent News
About this writer
Stories
n/a
Since n/a
n/a
Anyone can write for us. We pay you weekly for each story we publish
Write for us!