Opinion
Hongera Matiang’i kwa kuwa mzalendo

Elimu ni kitu ambacho hakistahili kupoteza umuhimu wake katika jamii.

Jukumu la kueneza maadili mema katika nyanja ya elimu limekuwa kizungumkuti kwa Wakenya wengi.

Tangu wanafunzi watambue kuvuna shuleni bila kupanda, imekuwa vigumu kukadiria uwezo wa watahiniwa katika mitihani ya kitaifa.

Imetuchukua miaka mingi sana kupata Mkenya anayeenzi masomo yenye dhamana kama Waziri wa Elimu Fred Matiang’i.

Ikiwa atapewa muda wa kutosha wa kuwapa mwelekeo washika dau katika sekta hii, Kenya itakuwa ya kupigiwa mfano barani.

Matiang’i anastahili kutunukiwa sifa tele kwa sababu anayotenda yamezidi matarajio ya wengi.

Bwana huyu amejaribu kupunguza uhayawani wa serikali ya Jubilee. Wakati wengine wanaiba raslimali ya umma kwa bidii ya kuogofya, Matiang’i anawatumikia Wakenya walipa ushuru.

Barabara zetu zitadumu kwa sababu wahandisi watakuwa waliohitimu kwa haki. Aidha, hatutapoteza wananchi katika majumba yanayoporomoka kila siku.

Isitoshe, hospitali zitasheheni madaktari wenye ari ya kutibu wala sio walevi na wafisadi wanaowaua wagonjwa na kuavya mimba kiholela.

Vile vile, walimu watakuwa watu wenye wito wa kuwapa watoto wetu elimu bora.

Matiang’i amezuia maovu mengi. Kongole apewe bila kuingiza siasa kwa kazi yake nadhifu.

Matapeli wanapanga kumng’atua wizarani lakini Mola amulinde mzalendo huyu. 

Report Story
Recent News
About this writer
Stories
n/a
Since n/a
n/a
Anyone can write for us. We pay you weekly for each story we publish
Write for us!