[Photo/courtesy]Bunge la kitaifa pamoja na seneti zinakamilisha mihula yao leo. Wabunge wanatarajiwa kuelekeza macho yao katika kampeni za uchaguzi mkuu. Hayo yanajiri huku serikali za kaunti zikiwa katika hatari ya kukosa fedha za kuendesha shughuli baada ya mabunge hao kukosa kuafikiana kuhusu mswada wa ugavi wa mapato. Maseneta wamelishutumu bunge la kitaifa kwa kuhujumu jukumu lao la kuhakikisha serikali za kaunti zinatengwa mgao unaopaswa wa fedha. Kulingana na seneta wa Kiambu Kimani Wamatangi maspika wa mabunge yote mawili wanapaswa kupewa nguvu kikatiba kuamua kuhusu mijadala ya miswada mbali mbali ili kuepusha mivutano zaidi katika siku za usoni.

Share news tips with us here at Hivisasa