Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi. Awali.[Picha/standard.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku zikiwa zimesalia siku 5 kwa marudio ya uchaguzi wa uraisi kufanyika,bado viongozi wa NASA kaunti ya Mombasa wanashinikiza kutofanyika kwa uchaguzi huo.

Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amesisitiza kuwa hakutakuwa na uchaguzi kaunti ya Mombasa hadi pale matakwa ya NASA yatakapozingatiwa.

“Hakuna uchaguzi kufanyika Mombasa, hadi matakwa ya Nasa yatimizwe”,alisema Mwinyi.

Akizungumza eneo la Docks, siku ya Ijumaa, Omar amewataka wafuasi wa NASA kutoshiriki zoezi hilo la marudio ya uchaguzi wa uraisi mpaka Tume ya uchaguzi itakapowahakikishia wananchi kuwa uchaguzi huo utakuwa wa uwazi, huru na haki.

“Musijitokeze kabisa Oktoba 26, ndio uchaguzi usifanyike kamwe”,alisema Mwinyi.

Ameongeza kuwa bado Mombasa ni ngome ya Nasa, wala si ya Jubilee kamwe, hivyo hakuna uchaguzi kufanyika.

“Mombasa bado ni Nasa,si Jubilee, hakuna cha kura kufanyika”,alisema Mwinyi.