Mbunge wa Lamu Magharibi Stanley Muthama. [Picha/Facebook]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa Lamu wameombwa kujitokeza kwa wingi na kumpingia kura Uhuru Kenyatta Oktoba 26 kwenye uchaguzi wa uraisi.

Mbunge wa Lamu magharibi Stanley Muthama amewasihi watu wa Lamu, kujitokeza kwa wingi ili kupigia kura Jubilee.

“Raukeni kwa wingi mupige kura kwa Uhuru Kenyatta,aweze kushinda kwa kura nyigi,”alisema Muthama.

Aidha, amewataka wakazi wa Lamu, kuupuzilia mbali porojo za Nasa za kususia uchaguzi huo, kwa kusema Nasa imekosa mwelekeo.

“Nasa hawana mwelekeo wa maendeleo, musifate mambo yao,” alisema Muthama.

Naye Mwakilishi wa wanawake Ruweida Obo ameshtumu maandamano yanayopangwa kufanywa na muungano wa  NASA siku ya uchaguzi.

Ruweida ameyataja maandamano kama yanayozorotesha uchumi wa nchi. 

Wakati huo huo wamewasihi wakaazi kudumisha Amani kabla na baada ya uchaguzi huo wa urais.

Kampeni sawia na hizo zimeendelezwa katika kaunti ya Kilifi ambapo seneta maalumu katika kaunti hiyo Christine Zawadi akisema serikali imeleta miradi mingi ya kimaendeleo katika kaunti hiyo.

Christine amewataka wananchi kutopotoshwa na viongozi wa NASA kwa kile alichoeleza kuwa hawajawafanyia maendeleo yoyote wakazi wa Kilifi.