[Photo/courtesy]Chama cha walimu wakuu wa shule za upili nchini [KESSHA] kimewatuza walimu waliofanya vizuri kwa mwaka huu huku walimu wakike wakitawala tuzo za mwaka huu.Tuzo ya mwalimu mkuu bora wa mwaka 2017 ilimwendea Anastasia Amollo wa shule ya upili ya wasichana ya Lwak kutoka kaunti ya Siaya.Anastasia ambaye amekuwa katika taaluma ya ualimu kwa muda wa miaka 28 ametaja juhudi na kupenda kazi yake ya uwalimu ndio imekuwa chanzo kikuu kwa yeye kuibuka kuwa mwalimu mkuu bora huku pia jitihada za kuhamasisha motto wa kike zimeendelea kumpatia ufanisi zaidi.Tuzo la mwalimu bora wa mwaka lilimwendea naibu mwalimu mkuu Phylis Wangeci wa shule ya upili ya wasichana ya Mahiga kutoka kaunti ya Nyeri.Wangeci ambaye hufunza somo la Kiswahili hakuficha furaha yake huku akielezea amekuwa na bidii katika kazi yake na hilo limemfanya kupata ufanisi huo mkubwa.Walimu hao walituzwa wakati wakufungwa rasmi kwa kongamano la walimu wakuu wa washule za upili ambalo limedumu kwa muda wa siku tano mjini Mombasa

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know